Somo la Biblia
Masomo ya Msingi ya Biblia
Kozi hii inamfundisha mwanafunzi misingi muhimu ya Biblia kuhusu Mungu, asili ya mwanadamu, dhambi, wokovu, neema, sheria, Sabato, ubatizo, hali ya wafu, kurudi kwa Yesu mara ya pili, na tumaini la mbingu mpya na nchi mpya.
Kuhusu Somo Hili
Karibu katika kozi ya Masomo ya Msingi ya Biblia.
Kozi hii imeandaliwa kumsaidia mwanafunzi kuelewa misingi muhimu ya imani ya Biblia kwa njia rahisi, ya hatua kwa hatua, na yenye maswali ya kujipima uelewa mwishoni mwa kila somo.
Katika kozi hii utajifunza kuhusu Mungu na kusudi lake kwa mwanadamu, Biblia kama Neno la Mungu linaloaminika, asili ya dhambi, mpango wa wokovu, neema na sheria, Sabato, ubatizo, hali ya wafu, kurudi kwa Yesu mara ya pili, pamoja na ahadi ya mbingu mpya na nchi mpya.
Malengo ya kozi:
1. Kumsaidia mwanafunzi kumfahamu Mungu kama Muumbaji, Mtawala, Baba na mwenye upendo.
2. Kumfundisha mwanafunzi kwa nini Biblia ni Neno la Mungu linaloweza kuaminiwa.
3. Kueleza asili ya dhambi na matokeo yake kwa mwanadamu.
4. Kufafanua mpango wa wokovu kupitia Yesu Kristo.
5. Kueleza uhusiano kati ya neema, sheria ya Mungu, na maisha ya utii.
6. Kumsaidia mwanafunzi kuelewa Sabato, ubatizo, hali ya wafu, na tumaini la kurudi kwa Yesu.
7. Kumwandaa mwanafunzi kufanya maamuzi ya kiroho kwa kumkabidhi Yesu maisha yake.
Muundo wa kozi:
Kozi hii ina masomo 10. Kila somo lina mafundisho ya msingi, mafungu ya Biblia ya kusoma, video za kujifunza, na maswali ya kujipima uelewa.
Masomo yaliyomo:
1. Mpango wa Mungu na Asili ya Mwanadamu
2. Biblia, Kitabu Unachoweza Kukiamini
3. Anguko la Mwanadamu / Asili ya Dhambi
4. Mpango wa Wokovu
5. Neema na Sheria
6. Sabato
7. Ubatizo
8. Wafu Wako Wapi?
9. Kurudi kwa Yesu Mara ya Pili
10. Mbingu Mpya na Nchi Mpya
Baada ya kumaliza kozi hii, mwanafunzi atakuwa na uelewa mzuri wa mafundisho ya msingi ya Biblia na ataweza kuendelea kujifunza masomo ya juu zaidi kwa msingi imara wa kiroho.
Yaliyomo kwenye Somo
Fungua kila moduli kuona mada, majaribio, na hatua za kujifunza.
Mungu Mmoja wa Kweli
Sifa za Mungu
Tabia ya Mungu
Mwanadamu na Mahusiano Yake na Mungu
Mungu Alimuumbaje Mwanadamu?
Kusudi la Mungu kwa Mwanadamu
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Biblia Iliandikwa na Nani?
Biblia Iliandikwa Lini?
Faida ya Biblia kwa Mwanadamu
Ushahidi Kuwa Biblia ni Neno la Mungu
Biblia Iliandikwa kwa Ajili ya Nani?
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Shetani Alitokea Wapi?
Shetani Aliwadanganyaje Adamu na Hawa?
Dhambi ni Nini?
Adamu Alipoteza Nini Baada ya Dhambi?
Mtu Anayefanya Dhambi Anakuwaje?
Uamuzi wa Kumtii Mungu
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Wokovu ni Nini?
Mpango wa Wokovu Ulianza Lini?
Kilichohitajika Kuleta Wokovu
Ni Nani Anayeweza Kuokoa?
Ni Nani Atakayeokolewa?
Wanaokataa Mpango wa Wokovu
Mpango wa Wokovu Utakamilika Lini?
Jaribio la Moduli
Maswali 6 · Alama ya kufaulu 100%
Maana ya Sheria
Asili ya Sheria ya Mungu
Sheria Inavyopaswa Kutunzwa
Yesu Kristo na Sheria ya Mungu
Ukomo wa Sheria ya Mungu
Maana ya Neema
Neema Inatolewaje?
Nguvu ya Neema kwa Mwanadamu
Uhusiano wa Neema na Sheria
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 98%
Siku ya Ibada na Mapumziko
Siku ya Sabato ni Siku Gani?
Maagizo ya Mungu Kuhusu Sabato
Yesu Kristo Aliitunza Sabato
Mitume Waliitunza Sabato
Namna ya Kuitunza Sabato
Sabato ni Muhuri wa Mungu
Jaribio la Moduli
Maswali 7 · Alama ya kufaulu 100%
Hatua za Mwanadamu Ili Aokolewe
Maisha Mapya Ndani ya Kristo
Ubatizo wa Biblia ni wa Namna Gani?
Ubatizo kwa Kuzamishwa Majini
Baada ya Kubatizwa, Nini Kinafuata?
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Wafu Wako Wapi?
Mungu Alimuumba Mwanadamu kwa Kutumia Nini?
Kinachotokea Mtu Anapokufa
Hali ya Wafu Kulingana na Biblia
Uongo wa Kwanza wa Shetani Kuhusu Kifo
Udanganyifu wa Kuwasiliana na Wafu
Mungu Pekee Ndiye Asiyekufa
Tumaini la Ufufuo
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Ahadi ya Kurudi kwa Yesu
Wazee wa Agano la Kale Walizungumziaje Kurudi kwa Yesu?
Yesu Atakuja kwa Namna Gani?
Watu Watakuwa Wakifanya Nini Yesu Ajapo?
Je, Tunaweza Kujua Siku na Saa ya Kurudi kwa Yesu?
Dalili za Kurudi kwa Yesu
Nini Kitawatokea Waovu Yesu Ajapo?
Uamuzi wa Kujiandaa kwa Kurudi kwa Yesu
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%
Mpango wa Mungu wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya
Sifa za Yerusalemu Mpya
Mti wa Uzima Katika Mji Mpya
Yerusalemu Mpya Utashuka Duniani
Mwisho wa Waovu na Dhambi
Ahadi za Mungu kwa Watakatifu Wake
Watoto na Wapendwa Katika Nchi Mpya
Tutakuwa na Mwili wa Namna Gani?
Maisha Katika Nchi Mpya
Jinsi ya Kuwa na Uhakika wa Kuingia Katika Ufalme wa Mungu
Jaribio la Moduli
Maswali 5 · Alama ya kufaulu 100%