Kuhusu Sisi

KUHUSU
Uzima Milele

Uzima Milele ni Huduma ya Kikristo isiyo ya faida ambayo hutoa elimu ya Biblia, Afya na Jamii kupitia mifumo ya kidijitali kwa lugha ya Kiswahili, ikilenga zaidi ya watu milioni 100 wanaoishi katika nchi zinazozungumza Kiswahili Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Dira

Kupitia timu yetu mahiri ya wainjilisti, wachungaji, wamishonari wa afya, wataalamu wa teknohama na wabia wetu, Huduma za Uzima Milele zinaleta maarifa yabadilishayo maisha mikononi mwako. Mtu yeyote, mahali popote, wakati wowote ataweza kupata masomo ya biblia, elimu ya afya na maisha ya familia kwenye MTANDAO, kupitia mifumo yetu ya kidijitali. Tunaomba, na kuamini, kuwa kupitia Uzima Milele, mamilioni watapata amani na furaha katika maisha haya, na maarifa yakayowaongoza katika uzima wa milele.

Dhima

Yesu alisema, "Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10).  Hivyo, Dhima yetu ni kuwaongoza wengine kwa Yesu Kristo kupitia mifumo yetu ya kidijitali, na kuwasaidia waweza kupata:  kwanza, amani na furaha katika maisha haya, na pili, uhakika wa wokovu wao na uzima wa milele kupitia Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu.

Uzima Milele

Uzima Milele ni Huduma ya Kikristo isiyo ya faida ambayo hutoa elimu ya Biblia, Afya na Jamii kupitia mifumo ya kidijitali kwa lugha ya Kiswahili, ikilenga zaidi ya watu milioni 100 wanaoishi katika nchi zinazozungumza Kiswahili Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Image
Makazi
Dar-Es-Salaam, Tanzania
Namba ya simu
0764504284
Barua Pepe
info@uzimamilele.or.tz
Maswali na Majibu
 
Hatimiliki © Uzima Milele 2025. Haki zote zimehifadhiwa.

Search