
Lengo katika kitabu hiki sio kuleta habari mpya za kutisha zenye kushitusha juu ya Uamsho na Roho Mtakatifu. Ingawa utakapo kisoma utagundua ukweli mpya na wa muhimu sana. Lengo kubwa ni kukuongoza katika Neno la Mungu na maandiko ya Ellen G. White mpaka kwenye kanuni za kiroho zinazogeuza maisha.
Unapokuwa unasoma kwa kutafakari kila sura, pata muda wa kuwa na maombi ya tafakari juu ya matokeo halisi ya kile unacho kisoma. Kadiri unavyofanya hivyo, akili yako itakuwa wazi kuongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa kina utajiweka katika mazingira ya Uamsho wa Kiroho.
Hakuna kitu ambacho huenda kina umuhimu mkubwa sana kwa watu wa Mungu kuliko kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kwa nguvu ambayo ni zaidi ya Ile ya Pentecoste kwa ajili ya kumaliza kazi ya Mungu hapa Duniani. Jambo hili inapaswa liwe la kwanza kabisa kwa mtu mmoja mmoja maana Uamsho huanza na mtu binafsi, iwe ni mwanamke au mwanamme, mvulana au msichana wakati anapopiga magoti kumtafuta Mungu. Wewe pia unaweza kuwa huyo mtu mmoja anayeweza kutumiwa na Mungu kuleta Uamsho wa kiroho nyumbani mwako, kanisani kwako, shuleni kwako au katika jamii yako.
Hivyo kupitia kitabu hiki, kwa kujitafakari tumwombe Bwana atuamshe tena Kiroho ili tumalize kazi yake hapa. Aje atuchukue twende nyumbani.
Mwandishi: Mark Finley