
Waandishi wengi wameandika kwa ustadi mkubwa juu ya MAPISHI ya vyakula, lakini bado kuna upungufu wa maandishi yanayoainisha MAPISHI na Afya za watu. Vitabu vingi vyenye ujuzi wa vyakula vinauzwa madukani na mitaani lakini bado kuna uhaba mkubwa wa vitabu vinavyoelimisha jamii kuhusu uhusiano uliopo kati ya mapishi, afya ya mwili na akili.
Wasomi wengi wamefanya tafiti za hali ya lishe katika jamii zetu. Hata hivyo bado kuna uchache wa matokeo ya tafiti juu ya mapishi na afya yaliyowekwa katika lugha rahisi kusaidia jamii kuwa na uelewa na uwezo wa kushughulikia afya kwa faida ya familia zao. Kuna vitabu vingi vyenye picha za kuvutia vinavyozungumzia vyakula na mapishi lakini vingi vimeandikwa kibiashara zaidi kuliko kiafya.
Kitabu hiki kinakujia kwa kusudi moja muhimu: kukufahamisha viini lishe katika vyakula vya kawaida katika mazingira ya kitanzania. Hivyo kukusaidia kufanya uchaguzi mahususi wa vyakula sambamba na mapishi kwa faida ya afya yako na jamii inayo kuzunguka.
Kitabu hiki ni maalumu kwa ajili ya kuelimisha watu wa makundi yote hivyo hakuna kizuizi cha kutumia jumbe za kitabu hiki kufundishia watu popoteMwandishi: Silas Khabele