
Kwanini kitabu hiki ni Muhimu?
Ninaamini hivi karibuni tutaingia katika kipindi kikuu cha taabu ambacho ulimwengu wetu haujawahi kupitia. Uweza wa Mungu na nguvu za yule Mwovu vitadhihirishwa. Tunawezaje kujiandaa kwa tukio hili?
Bwana ametoa ujumbe wa kutuandaa kwa ajili ya wakati huu na atatoa wito wenye kuvutia sana kwa kila mmoja wetu.
Katika kitabu cha ufunuo tunasoma maneno haya, "kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya Mbingu mwenye Injili ya milele awahubiri hao wakaao juu ya Nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu mcheni Mungu na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliye zifanya Mbingu na nchi na bahari na chemi chemi za maji.” - Ufunuo 14:6-7
Je Injili ya milele ni nini? Je tunajiandaaje kwa hukumu? Tunamtukuzaje Mungu? Tunamwabuduje Muumbaji?
Majibu bora kabisa yatapatikana katika kitabu hiki. Kusudi la Mungu katika kukupatia ujumbe huu ni kumwezesha kutokomeza dhambi katika Maisha yako, kwamba kupitia Imani ya Yesu aweze kuleta Haki ya milele. (Daniel 9:24)
Kisha atawaambia watu wake, “hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao Amri za Mungu na Imani ya Yesu.” (Ufunuo 14:12)
Nakutakia usomaji mwema wa kitabu hiki.
Mwandishi :E .J. Waggoner & A .T.Jones