
Hivi karibuni nimegundua kwamba watu wengi zaidi na zaidi wanahangaishwa na siku zijazo. "Kuhangaishwa" linaweza lisiwe Neno linalotosha kubeba maana kwa uzito wake, wengi wao wana hofu. Wanaihofia dunia ambayo watoto wao watakuzwa ndani yake, au hata kuwa na hofu kwamba dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa inaweza isiwepo wakati huo. KITABU hiki hakihusu hofu, kinahusu TUMAINI.
Sina shaka kwamba hukuchukua kitabu hiki kwa sababu ukitaka kuogopeshwa na takwimu zote za kuogofya za maovu katika dunia yetu. Ukweli ni kwamba kitabu hiki kitakusaidia kupata TUMAINI. Tumaini kwa ajili ya leo, kesho na hata milele. Kila sura ya kitabu hiki imejazwa na ujumbe wa matumaini katika kurasa hizi na utamfahamu Mungu anayekupenda zaidi ambavyo unaweza kutambua.
Mungu huyu anao mpango wa ajabu kwa ajili ya Maisha yetu. Utasoma kuhusu Mpango wa Mungu wa wokovu kwa ajili ya sayari hii yenye ugaidi na kuelewa kwa ukamilifu zaidi matukio yanayojitokeza katika dunia yetu hata sasa. Lakini bora kuliko yote, utapata ufahamu wa Mungu kutoka katika Neno la Mungu kuhusu jinsi dunia hii itakavyo koma.
Mwisho wa magonjwa, huzuni, machozi na Mauti unakuja punde, kwa kuwa Yesu ametuahidi dunia mpya kabisa. Punde anakuja kutuchukua kwenda nyumbani, na hii ndio mada ambayo kitabu hiki kinatatua. Hivyo kitafute ukisome ili ujazwe na Matumaini.
Mwandishi: Mark Finley