
Mwandishi wa kitabu hiki anasema anashauku kubwa kwa ajili ya vijana, na anatamani sana kuwaona wakijitahidi kukamilisha tabia zao za kikristo, kwa kujifunza kwa bidii na Maombi ya dhati, kupata Mafunzo Ambayo ni Muhimu kwa ajili ya huduma inayokubalika katika kazi ya Mungu. Anatamani sana kuwaona Vijana wakisaidiana ili wafikie kiwango cha juu cha uzoefu wa kikristo.
Kristo alikuja kuwafundisha wanadamu njia ya wokovu na alielezea njia hii kwa uwazi mkubwa kiasi ambacho hata mtoto mdogo anaweza kuipitia. Anawaagiza wanafunzi wake watafute kumjua Mungu na Kwa kadri wanavyofuata uongozi wake kila siku, watagundua kuwa msaada wake uko tayari daima kama ilivyo asubuhi.
Vijana wanahitaji kuweka mbele yao daima njia ambayo Kristo aliifuata, katika kila hatua ilikuwa njia ya ushindi. Kristo hakuna duniani kama mfalme kutawala mataifa, alikuja akiwa mnyenyekevu, alijaribiwa na alishinda majaribu ili kumfuata, inatupasa kumjua Bwana, kwa kujifunza maisha yake tutajua kile ambacho Mungu, kwa njia ya Kristo anaweza kuwafanyia watoto wake. Na tutagundua kuwa hata kama Majaribu yetu ni makubwa kiasi Gani, hayawezi kuzidi yale ambayo Kristo aliyashinda ili tuweze kujua njia na kweli na uzima. Kwa kuzingatia mfano wake, inatupasa kuonyesha shukrani kwa ajili ya kafara yake kwa ajili yetu.
Vijana wamenunuliwa kwa gharama isiyopimika yaani damu ya mwana Wa Mungu. Fikiria kafara ya Baba kwa kuruhusu Mwanawe kutoa kafara hii. Fikiria kile ambacho Kristo alikiachia alipoondoka ikulu mbinguni na kukiacha kiti cha kifalme, ili kutoa maisha yake yawe kafara ya kila siku kwa ajili ya wanadamu. Aliaihishwa na kutukanwa. Alibeba matusi na dhihaka ambazo watu waovu walimtwisha. Na utumishi wake duniani ulipokamilika, alikufa kifo cha msalaba. Fikiria mateso yake Msalabani misumari ikipigiliwa katika viganja vyake na nyayo zake kebehi na dharau kutoka Kwa wale aliyokuja kuokoa kufichwa uso wa Baba yake. Lakini ni kwa njia ya mambo haya Kristo anawawezesha watu wote wanaompenda wawe na uzima wa milele.
Mwandishi: Ellen G. White